AMREF TANZANIA KUENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI KUPITIA UFADHILI WA SERIKALI YA MAREKANI

  

Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi na Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), Dkt. Anath Rwebembera (katikati) mgeni rasmi, (kulia) Dkt. Liberate Mizoh- Naibu Meneja Programu wa NTLP Wizara ya Afya (Kushoto) Dr Edwin Kilimba Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti Amref Tanzania

 

Meneja Programu wa NASHcop, Dkt. Anath Rwebembera (katikati) mgeni rasmi, (kulia) Dkt. Liberate Mizoh- Naibu Meneja Programu wa NTLP Wizara ya Afya (Kushoto) Dr Edwin KIlimba Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti Amref Tanzania, wakati wa mkutano wa Utambulisho wa Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU (Afya Thabiti) na Wizara ya Afya na TAMISEMI ulioandaliwa na Amref Health Africa Tanzania Tarehe 26 Januari 2024, Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Dodoma


Mradi wa Afya Thabiti unafadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania katika mikoa ya Tanga, Simiyu, Mara Pamoja na Zanzibar una lenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ilikuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la Ukimwi nchini.
Meneja Programu wa NASHcop, Dkt. Anath Rwebembera (katikati) mgeni rasmi, (kulia) Dkt. Liberate Mizoh- Naibu Meneja Programu wa NTLP Wizara ya Afya (Kushoto) Dr Edwin KIlimba Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti Amref Tanzania, wakati wa mkutano wa Utambulisho wa Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU (Afya Thabiti) na Wizara ya Afya na TAMISEMI ulioandaliwa na Amref Health Africa Tanzania Tarehe 26 Januari 2024, Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Dodoma


#Mradi wa Afya Thabiti unafadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania katika mikoa ya Tanga, Simiyu, Mara Pamoja na Zanzibar una lenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ilikuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la Ukimwi nchini.


***

Dodoma, Tanzania - Januari 26, 2024 - Shirika la Amref Health Africa, Tanzania Leo imefanya Mkutano na Wizara ya Afya na TAMISEMI wenye lengo la kutambulisha Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU ujulikanao kama Afya Thabiti.

Mradi huo unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania na timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mikoa ya Simiyu, Mara na Visiwani Zanzibar unalenga lenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI nchini.

Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Afya na TAMISEMI na ulifunguliwa na Dkt. Anath Rwebembera, Meneja wa Programu ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi na Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) alisema "Wizara ya Afya na serikali kwa ujumla imeendelea kufanya kazi na wadau katika kutekeleza afua mbalimbali za kiafya, kuboresha miundombinu na kutoa huduma za afya kwa walengwa. Serikali imejipanga kuhakikisha inafikia lengo la dunia la kutokomeza janga la UKIMWI ifikapo 2030. Ndiyo maana leo hii tuko na wadau wetu hapa Amref Tanzania, ambao wamekuwa kiungo muhimu katika kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na kuwalinda ambao hawajapata maambukizi ya VVU wasiambukizwe."


Akizungumza na washiriki, Dkt. Anath Rwebembera alisema "Kiwango cha maambukizi ya VVU kwa Tanzania ni Asilimia 4.4 (Tanzania Bara 4.5, Zanzibar 0.4). Maambukizi yameendele kuwa makubwa Zaidi kwa mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Kagera, Shinyanga, Ruvuma, Geita, Pwani, na Mwanza ambapo maambukizi yako juu ya kiwango cha maambukizi kitaifa kwa mujibu wa THIS 2023. Aidha kiwango cha maambukizi mapya ni kikubwa kwa Mwaka kwa Vijana kimeonekana kuwa asilimia 0.18 sawa na visa 60,000 huku maambukizo kwa vijana wa kike yanaonekana kuwa asilimia 0.24 ikilinganishwa na 0.11 ya vijana wa kiume.


"Hata kiwango cha jumla cha maambukizi kinaonesha asilimia 5.6% ni wanawake ikilinganishwa na 3.0 miongoni mwa wanaume. Hata hivyo kiwango cha maambukizi kimeendelea kimeshuka ukilinganisha na miaka mitano iliyopita kutokana na juhudi na hatua ambazo zimeendelea kufanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau”, aliongeza Dkt. Anath Rwebembera.


Akizungumza na washiriki, Dkt. Anath Rwebembera alisema “ Leo hii katika kuendeleza wajibu wake na kuunga mkono jitihada za serikali, Shirika linatekeleza mradi wa Afya Thabiti kuanzia October 2023 mpaka Sept 2028 katika mikoa ya Mara, Simiyu Pamoja na Zanzibar. Matarajio ya serikali ni mradi kuendeleza mafanikio ya miaka 5 iliyopita na kuendelea kupunguza au kumaliza maambukizi mapya kwenye maeneo ya mradi.

Serikali itaendelea kushirikiana na mradi na kutoa kila aina ya mchango unaotakiwa ili mradi wa Afya Thabiti uweze kupiga hatua kubwa Zaidi. Mradi utaendelea kupata ushirikiano kuanzia wizara na timu za usimamizi wa afya katika mikoa na maeneo husika” alisisitiza.


Kwa upande wake, Daktari Edwin Kilimba, Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti, akimwakilisha Daktari Florence Temu, Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Tanzania alisema " Tunaamini ushirikiano wa karibu na wenzetu katika mikoa ya Mara na Simiyu utatusaidia kufanikisha lengo la serikali katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wote."

Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita yaani 2018 mpaka 2023, Amref Health Africa Tanzania tulitekeleza mradi wa tiba na matunzo wa Afya Kamilifu chini ya ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC Tanzania katika mikoa ya Tanga, Simiyu, Mara Pamoja na Zanzibar.

Aidha, Mradi ulifanya vizuri wakati lilipozuka janga jingine la COVID-19 kwa kuhakikisha huduma za tiba na matunzo zinaendelea na kuwalinda watu wanaoishi na VVU dhidi ya COVID-19. "Kwa kipindi cha uhai wa mradi wa Afya Kamilifu uliomalizika, Shirika liliweza kuibua visa vipya 78,877, kuwaunganisha huduma 173,305 na pia asilimia 99 ya walioanzishiwa dawa walishusha wingi wa Virusi",alisema Dr.  Edwin Kilimba.


Amref Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wizara zote, mashirika ya serikali, wafadhili, mashirika ya kijamii (CBOs), mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), sekta binafsi, na wanajamii. Katika kuchangia upatikanaji sawa na endelevu wa huduma bora za afya ya msingi (PHC) na hatimaye kuchangia katika kufanikisha huduma ya afya kwa wote (UHC) nchini Tanzania.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post