Mazingira ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Utawala na Madarasa ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Na Kadama Maunde - Malunde 1 blog
Maajabu ya Shule za Sekondari Little Treasures!! Hivi ndivyo unaweza kusema! Shule ya Sekondari Little Treasures (Little Treasures Secondary) iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imepata matokeo mazuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2023 kwa ufaulu mkubwa wa asilimia 100 ambapo wanafunzi wote 63 wamefanikiwa kupata daraja la kwanza na daraja la pili tu (Division One & Two tu pekee).
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kutangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2023, Januari 25,2024 Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures, Alfred Gikaro Nchagwa amesema wameyapokea matokeo kwa furaha kubwa.
“Little Treasures tumeyapokea matokeo ya Kidato cha nne 2023 kwa furaha kubwa sana, matokeo ni mazuri sana tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa, vijana wetu wamepambana na kwa msaada wa walimu na ushirikiano mzuri wanaotupatia wametuwezesha sisi kuwa na matokeo mazuri sana. Kwa hiyo haya ni matokeo mazuri, tunawapongeza sana vijana wetu, walimu na wazazi kwa ujumla”,ameeleza Nchagwa.
“Tumepata ufaulu mkubwa wa asilimia 100 kwa sababu wanafunzi wetu wote wamefanikiwa kupata daraja la kwanza na daraja la pili tu. Haya ni matokeo mazuri sana, ni kiwango ambacho tunasema ni kiwango ambacho ni kizuri kupita maelezo. Pia GPA imepanda ukilinganisha na mwaka 2022. Shule zetu za Msingi na Sekondari zinaendelea kufanya vizuri”,amesema Nchagwa.
Akifafanua zaidi amesema jumla ya wanafunzi waliofanya Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 walikuwa 63 ambapo wavulana ni 33 na wasichana 30, kati yao wanafunzi 44 wamepata Daraja la Kwanza na wanafunzi 19 wamepata Daraja la Pili na hakuna na Daraja la tatu wala daraja la nne.
“Siri kubwa ya mafanikio haya ni juhudi za wanafunzi wetu na kujituma kwa walimu, kwa kweli tuna walimu wazuri sana pamoja na ushirikiano mzuri wa wazazi wanaotupatia. Lakini kubwa zaidi ni Mungu,siku zote tumekuwa tukimtanguliza Mungu kwa kila jambo, bila Mungu tusingefika hapa tulipo”,ameeleza Nchagwa.
Amebainisha kuwa shule hiyo imekuwa ikiwajengea uwezo wanafunzi wasio na uwezo kwenye baadhi ya masomo hivyo kuwezesha wanafunzi wote kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.
“Sisi Little Treasures tunatambua kuwa kila mwanafunzi ana uwezo, pamoja na changamoto zinazokuwepo hatuamini kwamba kuna wanafunzi ambaye hana uwezo wa kufanya vizuri, kwa hiyo tunachokifanya kwanza ni kutafuta mwanafunzi ana uwezo kwenye maeneo gani, na ukipata maeneo ambayo ana uwezo nayo ni rahisi kumjengea uwezo kwenye maeneo ambayo hafanyi vizuri. Hivyo tunawajengea uwezo ili wawe bora mwisho wa siku tunapata matokeo yanayoridhisha”,ameongeza.
“Shule ya Little Treasures ni shule ya kipekee sana, sisi hatujilinganishi na shule yoyote, tunajilinganisha sisi na sisi ina maana tunatafuta ubora kwa kujiangalia sisi.Tunaishi na vijana wetu kirafiki sana na kwa umoja sana hali ambayo inawajengea hali ya kujiamini sana”,amesema.
Amesema Shule ya Sekondari Little Treasures pia imeyapa kipaumbele masomo ya Sayansi kupitia mkakati waliojiwekea hali inayofanya shule hiyo iwe ya kipekee na kuendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ukizingatia kwamba masomo ya Sayansi na Teknolojia hayaepukiki katika ulimwengu wa sasa.
“Sisi sera yetu ni kila mwanafunzi ana uwezo wa kupata A kwenye kila somo, tunaendelea kutekeleza malengo yetu na tunatamani wanafunzi aweze kupata daraja la kwanza ya Pointi 7, tunaendelea kuboresha kwenye maeneo ambayo bado hayafanyi vizuri. Tunaamini kuwa ukiwa na malengo tangu mwanzo na ukajua unataka kufikia malengo yapi unaweza kufanya chochote kile, unaweza kukumbana na changamoto yoyote ile lakini mwisho wa siku ukafikia matokeo yako yale umejiwekea”,amesema.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures, Alfred Gikaro Nchagwa akizungumza kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne 2023
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Utawala na Madarasa ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Muonekano wa sehemu ya Madarasa ya Shule ya Sekondari Little Treasures
Muonekano jengo la Utawala la Shule za Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School na Little Treasures Secondary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)

Sehemu ya kupumzikia wageni katika shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School)
Mazingira sehemu ya shule ya Awali na Msingi Little Treasures (Little Treasures Pre & Primary School).
0 Comments