Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amemkabidhi shilingi Milioni kumi (10) Bi. Happyness Msanga ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba baada ya halmashauri hiyo kuwa kinara katika matumizi bora ya mfumo wa NeST katika mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara, Taasisi pamoja na Mashirika ya Umma.
Fedha hizo zimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma Tanzania (PPRA) kama motisha kwa Taasisi za Serikali kutumia mfumo huo katika manunuzi ya umma.
0 Comments