SHULE YA SEKONDARI KOM YANG'ARA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2023

Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ni shule inayosifika vizuri kitaaluma kutokana na kuendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.

Kufuatia Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Januari 25,2024, Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi amesema matokeo hayo yamewaacha vizuri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 26,2024, Koyi amesema kati ya wanafunzi 142 zaidi ya wanafunzi 135 wanatarajiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

“Matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 sisi KOM yametuacha vizuri kutokana na tulivyokuwa tunawaandaa watoto na aina ya watoto tuliokuwa nao, tumefaulu kwa kiwango kikubwa kwa mfano tunategemea kupeleka Kidato cha Tano watoto zaidi ya 135 ambayo ni sawa na asilimia 96 ya wanafunzi wote 142 waliofanya mtihani, hili ni jambo la kujivunia kwani zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaenda High Level kutoka kwenye shule moja”,ameeleza.

Koyi amesema mafanikio makubwa yanayoonekana KOM yanatokana jitihada zinazofanywa na walimu na wanafunzi lakini pia kutokana na kwamba KOM inachukua wanafunzi wa kawaida kabisa na wanafanya vizuri kwenye mitihani baada ya kuwaongezea thamani.

Ameeleza kuwa KOM Secondary imekuwa ikipokea wanafunzi wa kawaida kabisa ambao wamepunguzwa kwenye baadhi shule hivyo wanajivunia kuona wanafunzi waliokataliwa mahali pengine wakienda hapo KOM wanawaongezewa thamani na wanafaulu vizuri kwenye mitihani na kuendelea na elimu ya kidato cha tano.

“Matokeo tumeyapokea vizuri na tumejaribu kufanya uchambuzi watoto wetu wameendelea kufanya vizuri zaidi na wengine wame Improve (wamekuwa na mabadiliko) zaidi. Kwa kweli sisi tunajivunia ufaulu wa vijana wetu ukizingatia KOM tupo tofauti na shule zingine, kulikuwa na suala la kupunguza watoto. Sisi hatupunguzi watoto kwa mfano kwa hili darasa la kidato cha nne lililomaliza mwaka 2023 tulianza tukiwa na wanafunzi 78 na tumemaliza tukiwa na wanafunzi 142, hii inaonesha kuwa badala ya watoto kupungua, sisi watoto wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka”,amesema Koyi.
“Katika sera za baadhi ya shule wanasema mtoto asipofika wastani flani anapunguzwa. Kwa sisi KOM wanafunzi ambao hawajafika wastani tunaamini kwamba tukiwachukua tunawaongezea thamani na hawa wanafunzi ambao wamekuwa wakiongezeka katika shule yetu, wengi wao wamepunguzwa kwenye shule zingine zenye sera ya kupunguza wanafunzi ambao hawajafikia wastani flani lakini sisi tunawachukua na kuwaongezea thamani na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani”,ameongeza Mkurugenzi huyo wa KOM Secondary School na Kom Pre & Primary School.

Katika hatua nyingine amewaomba wazazi kuwa na mwamko wa kupeleka wanafunzi shule huku akiahidi kuwa KOM itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwapa mafunzo walimu hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mtaala mpya wa masomo kwa kidato cha kwanza.

Mawasiliano zaidi KOM Secondary School

+255 767 618 213
+255 768 105 820
+255 767 483 046

Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi akizungumza kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023
Mkurugenzi wa Shule za Msingi KOM na Shule ya Sekondari KOM Jackton Koyi akizungumza kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023
Muonekano sehemu ya mazingira ya Shule ya Sekondari KOM iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga

Picha na Kadama Malunde 1 blog

Bofya Hapa Kutazama  Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne(CSEE) 2023 na Mtihani wa Maarifa (QT)

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post