WABUNGE SIMBA NA YANGA KUKIWASHA DODOMA

 


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Timu ya Wabunge na watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoshabikia timu hasimu za Simba na Yanga wanatarajia kukiwasha katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa Januari 27 mwaka huu kwa kuhusisha michezo 23 ambayo yote itachezwa kwa muktadha wa timu za  Simba na Yanga. 

Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Bunge Festo Sanga  amezungumza hayo leo Januari 25,2024 Jijini hapa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kuwa  hilo ni moja ya pambano ambalo litachezwa katika bonanza lililodhaminiwa na Benki ya Azania.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Spika Bungeni jijini Dodoma, Sanga ameeleza kuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambapo Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanatarajiwa kushiriki .

Amefafanua kuwa katika bonanza hilo kutakuwa na bonanza hilo ni maono ya Spika Dkt.Tulia ambapo lengo kubwa ni kuinarisha mahusiano baine ya watani wa jadi,wabunge ,taasisi mbalimbali pamoja na kuimarisha afya . 

"Benki ya Azania imeona ni vyema watunga sera wadhamini pambano hilo ili wapate fursa ya kujenga mahusiano na makundi mengine kupitia michezo."amesema 

Mkurugenzi Mhazini na Masoko ya Mitaji wa Benki ya Azania Gilbert Mwandamile  amesema Benki hiyo imedhamini bonanza hilo ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya michezo ikiwemo mpira na jezi. 

Naye Msemaji na Afisa Habari wa Timu ya soka ya Yanga Ally Kamwe amesema wapo pamoja na timu ya wabunge wanaoshabikia Yanga huku akisema ni furaha kwa Yanga kujumuika kwenye bonanza hilo huku akiwahamasisha wabunge kujipanga na kufanya vizuri katika mpambano huo.

Amesema, "Kesho tunafunga ofisi Jangwani tunahamia Dodoma ,hatutaki kucheza na mtu ,maana sisi ikishawekwa logo ya Yanga mahali ,shughuli hiyo tunaichukulia kwa umuhimu mkubwa ,kwa hiyo wabunge nendeni mkautwange susi tupo nyuma yenu."

Akizungumza kwa niaba ya Timu ya Simba Ally Shatry amewaasa mashabiki wa Simba wajitokeze katika pambano hilo huku akisema Simba hawanaga shughuli ndogo.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post