Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme anatarajia kufanya ziara ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitatua katika Manispaa ya Shinyanga, Kahama na Halmashauri ya Msalala kuanzia Februari 28 hadi Machi 1,2024.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Februari 27,2024, Mhe. Mndeme amesema Februari 28,2024 atasikiliza kero za wananchi Soko Kuu ,kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga kuanzia saa tano asubuhi.
"Februari 29,2024 kuanzia saa tano asubuhi nitasikiliza kero za wananchi katika kata ya Majengo Manispaa ya Kahama. Machi 1,2024 nitakuwa Kata ya Kakola Halmashauri ya Msalala na kuanzia saa nane mchana siku hiyo nitafanya mkutano wa hadhara katika kata ya Segese Halmashauri ya Msalala", amesema Mhe. Mndeme.
0 Comments