Hello mdau wa habari
Pokea salaam kutoka Twaweza, MISA-TAN, Jamii Forums, UTPC na TAMWA - Kwa umoja wetu tunakualika kuhudhuria Uzinduzi wa Sauti za Waandishi, ambapo tutakuwa tukijadili uzoefu na maoni ya waandishi wa habari wa Tanzania kuhusu sekta ya habari nchini Tanzania. Uzinduzi utafanyika Ijumaa, tarehe 16 saa 2:00 asubuhi - saa 7:00 mchana, katika Ukumbi wa Protea (Sea View) Jijini Dar es salaam. Tutakuwa live pia kupitia The Chanzo, na Haki TV. Tumeweka utaratibu mzuri kuhakikisha watakaokuwa online watapaza sauti zao na zitasikika katika mjadala. Hivyo uwe huru kushiriki online.
Miongoni mwa mambo machache yaliyobainika katika utafiti huu ni:
📝Asilimia ishirini tu (20%) ya waandishi wa habari wanasema ajira yao ni ya kudumu.
📝Waandishi wengi (63%) wanasema ni vigumu kupata maisha mazuri kupitia uandishi wa habari.
📝Waandishi wa habari wa kike wanahisi mara nyingi hawatendewi haki ikilinganishwa na wenzao wa kiume.
📝Nusu (50%) ya waandishi wa habari wanaripoti kuwahi kutishiwa, kuteswa, au kushambuliwa katika kazi zao.
Ripoti kamili itatolewa kwa washiriki wote baada ya uzinduzi.
Kwa kuwa umekuwa mdau muhimu wa vyombo vya habari, tunaamini sauti yako kwenye tukio hili itakuwa na thamani kubwa.
Wasiliana na Annastazia Rugaba kwa simu nambari 0687 222 197 au barua pepe arugaba@twaweza.org kwa maelezo zaidi.
Wasalaam
Annastazia kwa niaba ya waandaaji
0 Comments