MBUNGE WA TARIME MJINI MHE MICHAEL MWITA KEMBAKI AKABIDHI GARI LA WAGONJWA (AMBULANCE) KITUO CHA AFYA MAGENA

 
Na, Ernest makanya - Tarime Mara
 
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Michael Mwita Kembaki akiwa ameongozana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Ccm,  Madiwani pamoja Wananchi amefanikiwa kukabidhi Gari la Wagonjwa Kituo cha Afya Magena kisha kufanya Mkutano wa hadhara Magena Senta 13/2/2024.
Mhe Kembaki ametumia Mkutano huo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwajinsi anavyo watumikia Watanzania hasa wa Tarime kwa sababu kila kukicha Maendeleo yanazidi kuonekana na leo Mhe Rais ametupa Gari la Wagonjwa (Ambulance) hii kwa ajili yetu hivyo tutaitumia bure.

Nitumie nafasi hii kumpongeza Mganga Mkuu wa Magena kwa kazi kubwa anayo ifanya kwa sababu hakuna malalamiko yoyote katika Kituo Cha Afya Magena, Kituo hiki kimetusaidia kupunguza msongamano wa Wagonjwa katika Hospital  yetu ya Mji kwani zaidi ya Wagonjwa 840 hutibiwa katika Kituo hiki kila mwezi."
Alisema Mhe Kembaki.

Mhe Kembaki ameongeza kwa kusema mapungufu yote yaliyo jitokeza atayachukua na kuyafikisha kwa Waziri wa Afya.

Kupitia Mkutano huo Mhe Kembaki ameweza kuelezea mambo mbalimbali ikiwemo ufafanuzi wa Matumizi ya Mfuko wa Jimbo lakini pia kuwakumbusha Jinsi alivyo weza kuisaidia kata ya Nkende na Jimbo la Tarime Mjini kabla ajawa Mbunge na kuwasihii Wananchi waendelee kumwamini kwa sababu ni Mchapa kazi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime ambae ni Diwani wa Kata ya Nkende Mhe Daniel Komote amewaeleza wazi Wananchi wa Kata ya Nkende kwa kile alicho kifanya kama Diwani kwa miaka ambayo amewaongoza na kuwataka kuendelea kua na imani na Chama Cha Mapinduzi CCM.
"Wakati anaingia madarakani tulichaguliwa mafiga matatu kwa maana ya Rais, Mbunge na Diwani wakati huo yapo ambayo tuliweza kuahidi mfano Wakati tunaingia tulikuta Shule za Msingi 4 na sasa tunazo Shule za Msingi 10, tulikua na Sekondari 1 kwa sasa tunazo Sekondari 3, wakati tunaingia tulikua na Zahanati moja ya Magena kwa sasa tunacho Kituo cha Afya Magena na leo tumekuja kukabidhi Gari la Wagonjwa kutoka kwa Mhe Rais.
Alisema Mhe Komote.

Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Kituo Cha Afya Magena Mganga Mkuu ameweza Kumshukuru Mhe Rais, Mbunge na Diwani kwajinsi wanavyo kipambania Kituo cha Magena nakuwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaamini Viongozi hao kwa sababu ni wachapa kazi.

Mhe Kembaki Ameondoka Jimboni kuelekea Dodoma Kuendelea na Majukumu ya Kibunge
 



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post