Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ad Code

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI AGUSWA NA MSIBA WA HAYATI LOWASSA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa Ndg  Fadhiri Rajabu Maganya ameeleza ni kwa namna gani ameguswa na msiba  wa aliye wahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania Hayati Edward Ngoyai Lowassa aliye patwa na mauti tarehe 10.02.2024

"Tumepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa alikuwa kada wetu amekuwa kiongozi wetu kwa nafasi kubwa ya kitaifa na amefanya mengi kwenye Taifa hili hivyo tutamuenzi  kwa mazuri yake" Amesema Mganya
Aidha Mzee maganya ameelezea urafiki wap ulipoanzia kuwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa amekuwa rafiki yake  tangu walipokutana  kwa mara ya kwanza Mkoani  Arusha alipo kuwa amealikwa kama mgeni rasmi.

"Siku hiyo tuliweza kubadilishana namba za simu na tukawa tukiwasiliana mara kwa mara na nikawa namtania juu ya kugombea nafasi fulani na akawa ananishauri mbinu za kutumia, hata hivyo nitamkumbuka Lowassa kwa utulivu wake kwenye siasa amekuwa mwana siasa ambaye hakupendelea sana kusema sana na hata alipolazimika kuzungumuza juu ya jambo fulani amekuwa akitoa jibu la "No comment "  Amesema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Makanya amekiri kutambua mchango wa hayati Edward Lowasa katika Jumuiya hiyo na kwamba taifa limempoteza kiongozi mahiri na mchapa kazi kwani amekuwa akijitoa kwa manufaa ya Taifa.

"Sisi kama Jumuiya tunatambua mchango wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa kwenye Taifa hili kama Taifa tumepoteza kiongozi mahiri na mchapakazi, enzi za uhai wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa amekuwa akijitoa kwa mambo mbalimbali yenye manufaa na Taifa letu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com

Post a Comment

0 Comments