VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI VYATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA.

Na, Mwandishi Wetu - Dodoma.
 
Vituo vya kutolea huduma za afya nchini vimetakiwa kutoa Huduma Bora ili kuepuka malalamiko ambayo yanatia dosari za kiutendaji zinazoichonganisha serikali na wananchi wao ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti katika kila mwaka wa fedha kwaajili ya kununua mafuta kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulika na mambo ya Afya Dkt. Festo Dugange katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.

"Tuzingatie utoaji wa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum hasa Albino, tengeni bajeti ya mahitaji maalum kulingana na mahitai yao, utengaji wa fedha kwaajili ya mafuta maalumu kwa wenye ualibino ni maelekezo ya serikali na ni ya muhimu" Alisema Dkt. Dugange.

Naibu Waziri TAMISEMI anayeshughulikia mambo ya Afya Dkt. Festo Dugange akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.
 
 Amebainisha kuwa katika kipindi Cha miaka mitatu Halmashauri 47 tu zilitenga fedha kwaajili ya mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi, (Albino) hivyo ni vyema katika utoaji wa huduma kuwatambua ili wapate mafuta hayo yatakayowakinga na vitu mbalimbali.

Katika hatua nyingine amesema serikali haitamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atashindwa kusimamia usalama wa vifaa tiba vinavyopelekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kuboresha huduma za afya nchini.

"Ni jukumu lenu Waganga wafawidhi kuhakikisha  mnasimamia kwa ufanisi mkubwa vifaa tiba na kuvitumia kwa matumizi sahihi na si vinginevyo" Alisema Naibu Waziri Dugange

Akizungumza kwa niaba ya Waganga wafawidhi waliohudhuria mkutano huo Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara Dkt. Florence Hilari ameahidi kuzingatia maelekezo waliyopewa na kuyafanyia kazi kwa ufanisi na hatimaye kutoa Huduma bora na yenye tija kwa wananchi.

Dkt. Florence Hilari Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya Msingi Tanzania bara akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika Leo Februari 13, 2024 Jijini Dodoma.


Hata hivyo Mkutano huo wa siku mbili wa Mwaka wa Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Uwajibikaji ni Nguzo Muhimu katika utoaji wa huduma Bora za Afya ya Msingi"
 
 


 
















Post a Comment (0)
Previous Post Next Post